Featured post

HABARI KATIKA PICHA: ZIARA YA KWANZA YA MBUNGE WA KWANZA WA JIMBO LA ULYANKULU JOHN PETER KADUTU

MBUNGE WA ULYANKULU JOHN KADUTU AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI WA DINI VIONGOZI WA DINI WAKIFUATILIA HOTUBA YA MBUNGE WA ULYANKULU JOHN KADUT...

Friday, 11 December 2015

JE WAJUA? SIRI YA UTEMI KATIKA FAMILIA YA MTEMI MILAMBO?




Na Paul Christian,Ulyankulu.

Mzee Solomoni Kazwika Milambo ni mmoja wa wazee wachache wa ukoo wa Mtemi mashuhuri Milambo ambaye anaishi katika kijiji Usigala barabara ya 44 Ulyankulu mkoani Tabora.

Kijiji hicho cha Usigala kipo kwenye eneo ambalo linajulikana kama Ikonongo wakati wa utawala wa Mtemi Milambo.

Mzee huyo amezaliwa siku ya Jumatatu asubuhi ya tarehe 18, Julai mwaka 1945 na sasa ametimiza umri wa miaka 70.

Mnamo tarehe 28 Novemba, 2015 mzee Solomoni anakutana wa jopo la waandishi wa habari na kufanya mahojiano maalum kuhusu  sifa za mtu anayepewa Utemi katika ukoo wa Mtemi Milambo. 

Mzee huyo alisema, “Sisi kupewa Utemi inatokana na jinsi mtu alivyozaliwa au unabii unasemaje kuhusu mtu huyo.”

Alisema katika ukoo wa Milambo kabla ya Milambo hajazaliwa alianza Sibuga ambapo alipozaliwa ilishuka nyota moja, babu yake na Milambo aliyejulikana Kasele Muhofu aliongea akiwa bado tumboni mwa mama yake na ndio maana aliishi miaka 300, (1520-1820).

Mzee Solomoni alifafanua, “halafu alifuata shangazi Kibete alizaliwa akiwa malkia mwenye ziwa “titi moja” la mkono wa kushoto.”

“Mimi mwenyewe kabla ya kuzaliwa niliongea nikiwa tumboni mwa mama yangu na sikunyonya maziwa ya mama.” Aliongeza mzee huyo.

Mzee Solomoni alibainisha kuwa katika ukoo wa Milambo, mtu anayekabidhiwa mikoba ya Utemi ni lazima azaliwe kimaajabu au kuwe na unabii juu yake.

Alifafanua kuwa ikitokea akasimikwa Utemi mtu asiyetokana na maajabu au maelekezo maalumu hawezi kumaliza miezi miwili au mitano.

Siku hiyo ya Novemba 28, 2015, mzee Solomoni aliongoza jopo la wazee wa ukoo wa Milambo katika zoezi la kimila la kumsimika mbunge wa jimbo jipya la Ulyankulu John Peter Kadutu kuwa Mtemi.

Akizungumzia tukio hilo mzee huyo alisema kabla ya kumsimika mheshimiwa Kadutu nilioteshwa namna ya kumfanyia hivi na vila na kama nisingeoteshwa leo mvua isingenyesha.

Mzee Solomoni aliongeza “ndio maana mvua ilianza kunyesha kuanzia saa tatu asubuhi hadi muda ule tunafanya tambiko la kimila la kumsimika mheshimiwa Kadutu.”

No comments:

Post a Comment